JINSI YA KUTUMIA COMMCARE  KWA AJILI YA PATH CHW

 

Maelezo haya kwa ajili ya kuwasaidia watumiaji  wa CommCare wanaotumia simu, inaelekeza jinsi ya kutumia commcare kwa kutumia simu. Inaelezea vitu mbalimbali kwa kutumia  vielelezo tofauti ili mtumiaji aweze kuelewa kirahisi jinsi ya kutumia CommCare.Ni muhimu kusoma kielelezo hapo chini kwa makini ili uweze kuelewa vizuri jinsi ya kutumia simu hasa kwa wale ambao hawajawai kutumia simu hapo awali.

A. kitovu

B. kulia karibu na kitovu

C. Blue kulia

D. Juu karib na kitovu

E. Blue kushoto

F. kushoto karibu na kitovu

G. Kijani kushoto

H. Chini karibu na kitovu

I. Nyekundu kulia

 

 

 

 

s.02 Skrini

            

 

Bonyeza kitovu kwa ajili ya Menu. Shuka chini mpaka uone ‘ Applications’ bonyeza kitovu ili ufungue

 

          

Saa nyingine ukichukua muda kubonyeza kitovu taarifa  ya juu ndio inayojitokeza.Kurudi kwenye skrini iliyopita chagua back kwa kubonyeza Blue kulia h alafu bonyeza kitovu 

 

 

 

 

 

Shuka chini mpaka kwenye neno password ili uweze kuingiza namba yako ya siri (password) uliyopewa na mwalimu wako

Ukishaingiza namba yako ya siri ,utaona vinyota  vinatokea badala ya namba, hii itamzuia mtu mwingine asiweze kujua namba yako ya siri.

          

Ingia - Kama unatembelea mteja (mgonjwa) na taarifa unazoandika ni za mteja (mgonjwa) basi weka namba ya siri (password), hakikisha jila lako limeandikwa vizuri halafu shuka chini mpaka Ingia kama inavyonekana hapo juu halafu bonyeza kitovu ili kuingia kwenye  orodha ya fomu.

MAZOEZI - Kama unafanya mazoezi au majaribio (kwa maana nyingine taarifa unazoingiza sio za kweli basi huna haja ya kuandika nambari ya siri (password) shuka chini mpaka MAZOEZI halafu bonyeza  kitovu.

                      

Onyo la MAZOEZI - Ukifungua MAZOEZI utaona ukurasa hapo juu unafunguka ukiwa na maelezo bonyeza OK (Sawa).

      Tofauti kati ya Ingia na MAZOEZI

Labda unaweza kujiuliza kuwa kunatofauti gani kati ya Ingia na MAZOEZI ? Japo kuwa zote Ingia na MAZOEZI zinakuletea ukurasa wa ‘ Yaliyomo ’ lakini kuna tofauti ni kubwa sana.

-           Taarifa zote zinazoingizwa baada ya kubonyeza MAZOEZI huchukuliwa kuwa ni sehemu ya mazoezi na hazichanganyiki na zile zawateja.

-           Taarifa zinazoingizwa kwa kuweka nambari ya siri (password) huchukuliwa kuwa ni halisi na ni kumbukumbu za mteja (mgonjwa).

Yaliyomo - Ukurasa wa yaliyomo ni ule unaojitokeza kama hapo chini. Chagua huduma unayotaka kutoa, mfano; Mteja (mgonjwa), Taarifa ulizoingiza, unaweza kutuma taarifa ambazo hazijaenda na pia unaweza kutuma taarifa yako ya wiki.

Fig 1.                                       Fig 2.                             

          

  1. Mteja (mgonjwa) – Fungua fomu ya mteja (mgonjwa) iliuweze kufanya mambo mbalimbali yahusuyo mteja (mgonjwa), mf. Fomu ya kuandikisha, Fomu ya Dalili za Kifua kikuu.
  2. Fomu ya Elimu ya TB – Fungua hapa kila unapokwenda kuelimisha watu juu ya TB. Jaza fomu hii ilikuonyesha ni watu au makundi mangapi umeyaelimisha juu ya TB. Kumbuka kila baada ya kuelimisha unatakiwa kuona kama kuna mtu anahitaji kuandikishwa kama mteja kama ana dalili.
  3. Taarifa ulizoingiza- Fungua hapa iliuweze kuona taarifa ulizoingiza kwenye simu yako
  4. Tuma taarifa ambazo hazijaenda (0) -  Kama kunataarifa ambazo hazikwenda kwa sababu mbalimbali unaweza kuzituma kwa kufungua hapa

FOMU YA MTEJA (MGONJWA) HAPA CHINI

Ukifungua fomu ya Mteja (mgonjwa) utaona ukurasa kama huo hapo chini kushoto kwako unafunguka

                    Fig A.                                                     Fig B.                                                       Fig C.

=                      

Fig A. Sajili Mteja (mgonjwa) Mpya – Hapa unaweza kufungua maswali ya kumsajili mteja kwa mara ya kwanza

Fig B. Dalili za Kifua Kikuu- Hapa utafungua maswali ya dalili za kumuuliza mteja wako kuoa kama ana dalili za TB.

Fig C. Matokeo ya Rufaa (0)- Hapa unaweza kuangalia orodha ya wateja wote uliowapa rufaa, shusha hiyo rangi ya njano kama picha inavyoonyesha hapo juu kulia.  

Ujumbe wa onyo;

Ujumbe wa onyo - Utakapokuwa unajibu maswali kunawakati utaona ujumbe unatokea hasa pale utakapokuwa umeingiza kitu ambacho hakikubaliki kwenye hilo eneo. mfano hapa chini swali linauliza una miaka mingapi akasema 2, huwezi kumhoji mtoto wa miaka 2. Au endapo utaruka swali bila kulijibu, utapata ujumbe “ Swali hili lazima lijibiwe ”.

           

 

Jinsi ya kujibu maswali kwenye fomu mbalimbali za CommCare

Kujibu maswali - Kila unapomaliza kujibu swali bonyeza kitovu ili kwenda kwenye swali linalofuata.

Kutuma ujumbe - Ukimaliza kujibu maswali yote chagua ‘tuma sasa’.  Kama hakuna mtandao wa simu au simu yako haina hela basi chagua ‘tuma baadae’.

          Fig i.                                            Fig ii.                                            Fig iii.

        

Bonyeza kitovu ili uweze kutuma.

              Fig iv.